Masharti na sera
Masharti ya mauzo
- Unanunua leseni ya kutumia bidhaa ya kidigitali, si umiliki wa hakimiliki.
- Bei zinaonyeshwa kwa Shilingi za Tanzania (TZS) na zinathibitishwa na seva wakati wa malipo.
- Oda inakamilika pale tu mtoa huduma wa malipo anapothibitisha malipo. Picha ya skrini si uthibitisho wa malipo.
- Bidhaa ni zana za kupanga na kurekodi; si ushauri wa kisheria, kodi, uhasibu, kifedha wala kitabibu.
Sera ya marejesho
- Kwa kuwa ni bidhaa za kidigitali, hatutoi marejesho kwa kubadili mawazo baada ya kupakua.
- Tutarekebisha au kurejesha fedha kama: faili haifunguki, imeharibika, haikulingana na maelezo, au ulikatwa mara mbili kwa oda moja.
- Wasiliana nasi ndani ya siku 7 ukitaja namba ya risiti. Marejesho yanafanywa kupitia njia uliyolipia, kwa utaratibu wa mtoa huduma wa malipo.
- Fedha zikirejeshwa, link za kupakua za oda hiyo zinasitishwa.
Faragha na data zako
- Tunakusanya tu: namba ya simu ya malipo, email (kwa risiti na 'Bidhaa zangu'), na jina kama ukipenda.
- Hatukusanyi wala kuhifadhi PIN yako. PIN inawekwa kwenye simu yako tu.
- Tunatumia data kuchakata malipo, kutuma risiti na bidhaa, kutoa msaada na kuzuia udanganyifu. Hatuuzi data zako.
- Mtoa huduma wa malipo na mtoa huduma wa email wanachakata data zinazohitajika tu kwa huduma hizo.
- Takwimu za matumizi ya tovuti hazina taarifa binafsi (tukio, bidhaa, namba ya kivinjari ya bahati nasibu).
- Unaweza kuomba nakala au kufutwa kwa data zako, isipokuwa kumbukumbu za miamala tunazotakiwa kuhifadhi kisheria.
Leseni ya bidhaa
- Matumizi yako binafsi au ya biashara/kikundi kimoja.
- Unaruhusiwa kuhariri na kuchapisha kwa matumizi yako, na kutumia nyaraka ulizojaza na wateja wako.
- Huruhusiwi kuuza, kugawa, kupakia mtandaoni au kuweka template tupu kwenye bidhaa nyingine.
Malipo na usalama
- Malipo yanachakatwa na mtoa huduma wa malipo aliyesajiliwa (M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money).
- Namba binafsi ya muuzaji haionyeshwi; fedha zinaingia kwenye akaunti ya biashara iliyosanidiwa na mtoa huduma wa malipo.
- Kiasi kinachokatwa ni kile kinachoonyeshwa kabla ya kulipa. Mtandao wako unaweza kutoza ada yake ya kawaida.
Toleo / Version 4.0 · 2026-10-01